Return to Homepage

John 7:53-8:11 - Swahili/English Parallel Text


Walikwenda kila mtu nyumbani kwake;
naye Yesu akaenda mpaka hekaluni,


na watu wote wakamwendea;
naye akaketi, akawa akiwafundisha.

Waandishi an Mafarisayo wakamletea mwanamke aliyefumaniwa katika uzinzi, wakamweka katikati.

Wakamwambia,

Mwalimu, mwanamke huyu amefumaniwa alipokuwa akizini. Basi katika torati, Musa alituamuru kuwapiga kwa mawe wanawake namna hii; nawe wasemaje?

Nao wakasema neno hilo wakimjaribu, ilil wapate sababu ya kumshitaki.

Lakini Yesu akainama, akaandika kwa kidole chake katika nchi.

...And each person went to his own home, but Jesus went to the Mount of Olives.

And at Dawn Jesus came again into the temple, and all the people were coming to Him; and having sat down, He was teaching them.

And the scribes and Pharisees bring to Him a woman having been taken in an adultery;

And having set her in the midst,
They say to Him,
"Teacher! This woman was taken in the very act, - committing adultery;
and in the Law Moses commanded us that such be stoned to death;
You therefore, what do you say?"


And this they said testing Him, that they might have something to accuse Him of.'

But Jesus bent down and with the finger wrote upon the earth, ignoring them.

Nao walipozidi kumhoji, alijiinua, akawaambia, Yeye asiye na dhambi miongoni mwenu na awe wa kwanza wa kumtupia jiwe.

Akainama tena, akaandika kwa kidole chake katika nchi.

Nao waliposikia, wakashitakiwa na dharmiri zao, wakatoka mmoja mmoja, wakianzia tangu wazee hata wa mwisho wao;

akabaki Yesu peke yake, na yule mwanamke amesimama katikati.

Yesu akajiinua asimwone mtu ila yule mwanamke, akamwambia,
Mwanamke, wako wapi wale washitaki wako? Hakuna aliyekuhukumu kuwa na hatia?

Akamwambia,
Hakuna, Bwana.
Yesu akamwambia,
Wala mimi sikuhukumu. Enenda zako; wala usitende dhambi tena.

'And when they continued pressing Him, having bent back, He said to them,
"The sinless one among you -
Let him first cast a stone upon her!"

And again having leaned down, He was writing in the earth:

and they, having understood, being convicted by conscience, went forth one by one, beginning from the elders, even to the last.

And Jesus was left alone, and the woman standing in the midst of the crowd.

But Jesus, having bent Himself back, and seeing no one but the woman, said to her,
" ...where are those - your accusers? Did no one condemn you?"
And she said,
"No one, Lord."
And Jesus said to her,
"Neither do I judge you: Go, and sin no more."

(John 7:53-8:11)

The Swahili text has been exerpted for review purposes from
The Holy Bible in Swahili version of the NT, from the Bible Society of Kenya (1971).

The English is a modern rendering from the traditional Greek text (Textus Receptus) based upon the KJV (modernized), with corrections from Young's Literal Translation, and following the Greek text closely. Words of Jesus are in red, other dialogue is in blue.

Return to Homepage